Friday, September 20, 2013

SIO WASIKIAO, BALI WATENDAO.



SIO WASIKIAO, BALI WATENDAO.

1.      Ni kwa nini ahadi ilipewa Ibrahimu ya kuwa yeye na uzao wake watairithi nchi?
Kwa sababu Ibrahimu alisikia sauti yangu,akayahifadhi maagizo yangu,na amri zangu,na hukumu zangu,na sheria zangu.” Mwanzo 26:5.

  1. Ni na nani ndio Bwana ataweka agano, na kumuonyesha rehema?
Basi jueni ya kuwa BWANA,Mungu wenu,ndiye Mungu;Mungu mwaminifu,ashikaye agano lake na rehema kwao wampendao,na kushika amri zake hata vizazi elfu.” Kumbukumbu la Torati 7:9.

  1. Ni kwa nani ndiyyo Kristo anaelezea baraka?
       Lakini yeye alisema, Afadhali, heri walisikiao neno la Mungu na kulishika.” Luka 11:28.

  1. Je wote wasemao,’Bwana, Bwana’ wtaokolewa mwishowe?
     Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni;” Mathayo 7:21.

  1. Basi nani ataruhusiwa kuingia?
Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.” Mathayo 7:21.

  1. Ni visababu gani wengi watatoa katika siku hiyo kuu?
“Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?” Mathayo 7:22.

  1. Ni jibu gani watapokea?
Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mte­ndao maovu.” Mathayo 7:23.

  1. Watiifu wamefananishwa na nini?
“Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akiIi, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba.” Mathayo 7:24.

  1. Wale wasikiao neno, bali hushindwa kutii wamefananishwa na nini?
Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga.” Mathayo 7:26.

  1. Ni nani ndio Paulo anasema watahesabiwa haki?
Kwa sababu sio wale waisikiao sheria walio wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale waitendao sheria watakaohesabiwa haki.” Warumi 2:13.