Wednesday, June 12, 2013

MAPENZI YA MUNGU KUTUSAMEHE.



MAPENZI YA MUNGU KUTUSAMEHE.

1. Ni kwa njia gani Mungu ameshughulika na wenye dhambi?
  Hakututenda sawasawa na hatia zetu wala hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu” Zaburi 103:10.

2. Ni kwa nini ametushugulikia kwa namna hii?
  Kama vile baba awaoneavyo watoto wake ndivyo Bwana anavyowahurumia wamchao, kwa maana yeye anatujua umbo letu na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbiZaburi 103:13, 14.

3. Mungu yu tayari kufanya nini kwa wote wamwitao?
  Kwa maana wewe Bwana u mwema, umekuwa tayari kusamehe na mwingi wa fadhili kwa watu wote wakuitaoZaburi 86:5.

4. Wakati Ibrahimu alimwomba Mungu kusamehe Sodoma ikiwa angepata humo watu kumi watakatifu, Bwana alisemaje?
  Akasema Bwana asiwe na hasira nami nitasema mara hii tu, huenda wakaonekana humo kumi? Akasema, sitaharibu kwa ajili ya hao kumiMwanzo 18:32.

5. Ni ombi gani alilofanya Musa kwa niaba ya Israeli?
  Nakusihi usamehe uovu wa watu hawa kama ukuu wa rehema yako ulivyo kama ulivyowasamehe watu hawa tangu huko Misri hata hivi sasaHesabu 14:19.

6. Ni jibu gani Mungu alilolitoa muda huo huo?
  Bwana akasema  mimi nimewasamehe kama neno lako lilivyokuwaHesabu 14:20.

7. Wakati Daudi alipoungama dhambi yake kuu kwa Mungu, alipokea majibu gani?
  Nilikujulisha dhambi yangu, wala sikuuficha upotovu wangu, nalisema nitayakiri maasi yangu kwa Bwana nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu” Zaburi 32:5.

8. Je Mungu husamehe wakati wote dhambi zinapoungamwa kwa njia mwafaka?
  Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusatisha na udhalimu wote”. I Yohana 1:9.

9. Je utimilifu wa msamaha huu ni kiasi gani iwapo mtu atatimiza masharti?
  Mtu mbaya na aache njia yake, na mtu asiye haki aache mawazo yake, na amrudie Bwana naye atamrehemu na arejee kwa Mungu wetu naye atamsamehe kabisa” Isaya 55:7.

10. Ni kwa namna gani ya kipekee Mungu amedhihirisha nia yake kusamehe mwenye dhambi?
  Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi Warumi 5:8.

11. Je onyesho hili la ajabu la Mungu latufanya kutumaini vipi?
  Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutuki­rimia na mambo yote pamoja naye Warumi 8:32.

12. Ni kwa nini Mungu ametoa maafikiano haya?
  Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba II Petro 3:9.
.
13. Wakati mwana mpotevu katika mfano alipotubu na kurudi nyumbani, baba yake alifanya nini?
  “Akaondoka, akaenda kwa babaye. Alipokuwa angali mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia shingoni, akam­busu sanaLuka 15:20.

14. Alipouliza afanywe kuwa mmoja wa watumishi, ni amri gani iliyotolewa kwa sababu ya kutubu kwake?
  Lakini baba aliwaambia watumwa wake, Lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike; mtieni na pete kidoleni, na viatu miguuni; mleteni ndama yule aliyenona mkamchinje; nasi tule na kufurahi; kwa kuwa huyu mwanangu alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana. Wakaanza kushangiliaLuka 15:22-24.


15. Je Mungu ananuia kuwafanyia wanawe kama vile wazazi wa hapa duniani?
  Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?Luka 11:13.

16. Ni wangapi hupokea msamaha kutoka kwa Mungu?
  “…kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwaMathayo 7:8.

17. Je Mungu husahau vilio vya wale wamwitao?
  Je mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye…. Naam hawa waweza kusahau  lakini mimi sitakusahau weweIsaya 49:15.

No comments:

Post a Comment