Wednesday, June 12, 2013

SHERIA YATUKUZWA NA KRISTO.



SHERIA YATUKUZWA NA KRISTO.

  1. Taja haja ya Bwana kuhusu sheria?
 Bwana akapendezwa kwa ajili ya haki,kuitukuza sheria, na kuiadhimisha.” Isaya 42:21.

Kuitukuza-kuongezea nguvu au utukufu wa; kuinua, kuelezea sifa za-Webster.

  1. Ilikuwa na umuhimu gani kuitukuza sheria?
Wakati umewadia BWANA atende kazi;kwa kuwa wameitangua sheria yako.” Zaburi 119:126.

  1. Sheria ‘ilifanywaje tupu’ wakati Kristo alikuwa duniani?
      Akawaambia, Vema! Mwaikataa amri ya Mungu mpate kuyashika mapokeo yenu.” Marko 7:9
;Mathayo 15:1-9.



  1. Nia ya Kristo kuhusu sheria ilikuwa gani?
Msidhani ya kuwa nalikuja kutangua torati au manabii,La sikuja kutangua bali kutimiliza.” Mathayo 5:17. -Kuitimiza-kujalizia, kutimiza kama vile kufanya vyema-Greenfield Greek Lexiocon.Tazama pia Webster.Kristo, hivyo alikuja kutenda sheria vyema katika hali zote, wala si kama wayahudi walivyoitafsiri.

  1. Aliendeleaje kuitukuza sheria mbele ya wasikilizaji wake?
 Mmesikia watu wa kale walivyoa­mbiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu. Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.” Mathayo 5:21,22. Tazama pia 1 Yohana 3:15.

  1. Alisemaje kuhusu amri ya saba?
      Mmesikia kwamba imenenwa, Usizi­ni; 1akini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.” Fungu la 27,28.

  1. Je nia ya mwili yaweza kumtii Mungu na amri zake?
 Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheri a ya Mungu, wala haiwezi kuitii.” Warumi 8:7.

1 comment:

  1. New Slot Machine Games to Play on Steam! | Dr.MD
    Welcome 전주 출장마사지 to the world of Slot Machine Games! We 서울특별 출장샵 offer over 100 of the hottest new 당진 출장안마 slots, live table, and more. The latest and greatest games can be 계룡 출장마사지 found here 보령 출장마사지 at

    ReplyDelete