KUAMINI
KATIKA YESU.
- Nini ndio nabii wa Agano la kale alitabiri kuhusu Kristo?
“
Isaya 11:10.
- Ni vipi mtume alielezea unabii huu?
“Na tena lsaya anena, Litakuwako shina la
Yese, Naye aondokeaye kuwatawala Mataifa; Ndiye Mataifa watakayemtumaini.” Warumi
15:12.
- Mitume waliomuamini Kristo kwanza, walikuwa wawe akina nani?
“Nasi katika huyo tupate kuwa sifa ya utukufu
wake, sisi tuliotangulia kumwekea Kristo tumaini letu.” Waefeso 1:12.
- Nini ndio Waefeso walifanya waliposikia ujumbe wa kweli?
“Nanyi pia katika huyo mmekwisha
kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini
yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu”
Fungu la 13,sehemu ya kwanza.
- Ni matokeo gani walipokea kutokana na ukweli waliouamini?
“Nanyi
pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu;
tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye
Mtakatifu” Fungu la 13,sehemu ya mwisho.
- Ni kwa nani ndio injili inakuwa nguvu za Mungu?
“Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni
uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa
Myunani pia.” Warumi 1:16.
- Na ikiwa mtu atasitasita katika imani yake au kuamini; anachukuliwaje na Bwana?
“Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani;
Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.” Waebrania 10:38.
- Ni kupitia kwa nini ndio mtu anapata ushindi juu ya dunia?
“Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu
huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani
yetu.” 1 Yohana 5:4.
Shalom
ReplyDeleteam Samuel.
I have a question.
Why haven't you emblaced Sacred names?