Friday, September 20, 2013

KUAMINI KATIKA YESU.



KUAMINI KATIKA YESU.

  1. Nini ndio nabii wa Agano la kale alitabiri kuhusu Kristo? 
Isaya 11:10.

  1. Ni vipi mtume alielezea unabii huu?
Na tena lsaya anena, Litakuwako shina la Yese, Naye aondokeaye kuwatawala Mataifa; Ndiye Mataifa watakayemtumaini.” Warumi 15:12.

  1. Mitume waliomuamini Kristo kwanza, walikuwa wawe akina nani?
Nasi katika huyo tupate kuwa sifa ya utukufu wake, sisi tuliotangulia kumwekea Kristo tumaini letu.” Waefeso 1:12.

  1. Nini ndio Waefeso walifanya waliposikia ujumbe wa kweli?
“Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye MtakatifuFungu la 13,sehemu ya kwanza.

  1. Ni matokeo gani walipokea kutokana na ukweli waliouamini?
     “Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye MtakatifuFungu la 13,sehemu ya mwisho.

  1. Ni kwa nani ndio injili inakuwa nguvu za Mungu?
Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye,                      kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia.” Warumi 1:16.

  1. Na ikiwa mtu atasitasita katika imani yake au kuamini; anachukuliwaje na Bwana?
Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.” Waebrania 10:38.

  1. Ni kupitia kwa nini ndio mtu anapata ushindi juu ya dunia?
Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.” 1 Yohana 5:4.

1 comment:

  1. Shalom
    am Samuel.
    I have a question.
    Why haven't you emblaced Sacred names?

    ReplyDelete